Jinsi ya kureset simu/tablet ya android
Zifuatazo ni njia tatu unazoweza tumia
1. Kureset Kwa Kutumia Factory Reset
Hi ni njia rahisi kabisa ya kureset simu yako. kinachotakiwa ni kwenda kwenye Menu ya simu yako kisha unaenda kwenye Settings kisha unabofya Backup And Restore baada ya hapo unaenda kwenye Factory Reset. Kitu cha muhimu kujua hapa ni kwamba ukifanya hivi vitu vyako vitafutika hivyo ni muhimu kufanya back up ya data zako zote kabla hujafanya hivi.
kuna baadhi ya simu facory reset haipatikani kama ilivyoelekezwa hapo juu, nenda kwenye Privacy Settings
2. Kureset Kwa Kutumia USSD kodi
Watengenezaji wa simu wengi kama Samsung, HTC n.k huwa wanatoa kodi inayoweza ku ‘restore’ simu ya Android. Kodi hiyo ni *#7780# kwa hiyo kila utakapo piga hiyo kodi simu yako ya adroid itakuuliza kufomati. Ni vizuri kuback up data zako pia kwa sababu baadhi ya simu haziulizi ukipiga tuu hiyo kodi simu inaanza kufomati
3. Kureset Kwa Kutumia System Restore
Hi njia ya mwisho ni ngumu kidogo na haifahamiki sana laki ndio njia yenye nguvu kuliko hizo mbili hapo juu. Sifa za njia hii ni kwamba inafanya kazi hata simu yako ikiwa imeji ‘lock’ (kama umesahau pattern au password ya simu yako). Njia (1 na 2) hazitafanya kazi kama simu yako itakua imeji ‘loki’
JINSI
A. Zima Simu Yako Ya Android
Kama ni Mtumiaji Wa Samsung Bonyeza: Sauti juu + Home + Kuzima. Mara baada ya simu kunguruma achia kitufe cha kuzima. Mara simu ikiwa katika modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha sauti juu na cha home pia
Kama Ni Mtumiaji Wa HTC Bonyeza: Sauti Chini + Kuzima. Simu ikiwa inawaka achia kitufe cha kuwasha, ukiona imetokea modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha Sauti Chini
Kama Ni Mtumiaji Wa Micromax Bonyeza: Sauti Juu + Kuzima
SOMA PIA: Mkakati wa kuachana na magari yanayotumia mafuta waanza nchini Uingereza
B. Ukishaingia katika menyu ya System Restore tumia kitufe cha Sauti Juu Na Sauti Chini Kuchagua chaguo lako na kitufe cha kuwasha/kuzima simu kuchagua chaguo hilo
C. Sasa chagua chaguo lako kureset simu yako ya Android
Hii njia itachukua mda kidogo katika ufanyaji kazi wake laki unashauriwa kutotoa betri ya simu yako maana italeta hitilafu wakati wa kureset . Naimani njia hizi tatu zitakusaidia sana kureset simu ama tablet yako
Asante
Comments
Post a Comment